- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALMASHAURI 7 MATATANI KWA KULA HELA ZA UJENZI WA BARABARA.
DODOMA: Bodi ya mfuko wa barabara Tanzania imeziamuru halmashauri saba zilizotumia fedha zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara nchini na badala yake zikatumika kutengeneza madawati na ujenzi wa barabara zirejeshe fedha hizo ndani ya mwezi mmoja kabla hatua za kisheria zijachukuliwa.
Katika mwaka wa fedha 2015/16 bodi ya mfuko wa barabara nchini RFB kupitia wahandisi washauri ilifanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja ambapo jumla ya mikoa 22 na halmashauri zake zilikaguliwa
Akizungumza wakati akitoa taarifa ya ukaguzi wa kiufundi na fedha kwa kazi za ujenzi Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa barabara Joseph Haule ameziagiza halmashauri zilizofanya udanganyifu ambao ni kinyume naa taratibu kuzirejesha fedha hizo katika mfuko wa barabara huku zaidi ya shilingi ya shilingi milioni 64 zikitumika katika miradi hewa
Kwa upande wake meneja wa bodi ya mfuko wa barabara Eliud Nyauhenga amesema bodi hiyo imetoa muda hadi October 30 mwaka huu kwa halmashauri zilizotumia fedha hizo zirejeshwe kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa barabara
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara nchini wamesema kuwa kufuatia kuundwa kwa wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA kutawezesha kupunguza ubadhilifu wa fedha na mapato yanayotakiwa kutumika kwa ajili ya barabara.
Miongoni mwa halamshauri zilizotajwa kukiuka matumizi ya fedha za mfuko wa barabara na kupeleka kwenye madawati na ujenzi wa maabara ni halmashauri ya wilaya ya Karagwe,Kerwa,Ushetu,Masasi,