Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:26 pm

NEWS: HALMASHAURI 144 ZANUFAIKA NA RUZUKU ZA PEMBEJEO

DODOMA: KATIKA msimu wa kilimo wa mwaka 2015/2016 ,Serikali ilitoa ruzuku ya pembejeo kwa utaratibu wa vocha kwa mikoa 25 ya Tanzania Bara.
Akijibu swali Bungeni,Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha amesema,kazi ya kusambaza pembejeo hizo kwa kaya za wakulima wanufaika wapatao 999,926 ilifanywa na makampuni na Mawakala wa pembejeo katika Halmashauri zipatazo 144 zilinufaika na utaratibu huo.


Amesema,ili kujiridhisha na uhalali wa madai ya makampuni ya Mawakala waliotoa huduma ya pembejeo katika wilaya hizo,wizara hiyo imefanya uhakiki
wa awali ambao umefanyika katika baadhi ya mikoa yenye kiasi kikubwa cha madai.


Naibu Waziri huyo amesema kazi ya uhakiki wa awali umefanyika katika mikoa minane kati ya mikoa 25 ya Tanzania Bara iliyopata ruzuku .
"Matokeo hayo yameonyesha mapungufu makubwa katika madai hayo,"amesema.


Aidha amesema,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza wizara ya fedha na Mipango kufanya uhakiki katika mikoa yote kwa makampuni na mawakala wote waliosambaza pembejeo katika msimu wa 2015/2016 katika kipindi cha mwezi mmoja.


"Baada ya uhakiki huo madei yote halali yatalipwa." amesisitiza
Ole Nasha alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha (CCM) ambaye katika swali lake ,alitaka kujua mpango wa Serikali wa kulipa deni la shilingi milioni 824 ambalo mawakala waliosambaza pembejeo kwa vocha katika msimu wa mwaka 2015/2016 katika Halamshauri ya wilaya ya Mbinga wanaidai Serikali.