- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALIMA MDEE AMBANA WAZIRI ZUNGU UCHAFU DAR ES SALAAM
Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira nchini Tanzania, Mussa Zungu amekiri kweli dampo linalotumiwa na Jiji zima la Dar es Salaam lililopo Pugu Kinyamwezi lina hali mbaya.
Zungu amekiri hayo leo Alhamisi Januari 30, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe, (Chadema), Halima Mdee.
Halima ametaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kujenga dampo la kisasa jijini Dar es Salaam ili kutatua changamoto ya uchafu. “Je Serikali ina mpango gani kujenga dampo la kisasa kwenye maeneo mengine kila wilaya ili kuzuia uchafu kutokana na lililopo kutokidhi kubeba uchafu katika jiji zima,” amehoji.
Akijibu swali hilo, Zungu amesema kasi ya taka katika jiji hilo ni kubwa licha linakua kwa kasi na kwamba miaka ijayo linakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni nane hadi tisa na dampo ni moja