- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALIMA MDEE AITWA NA JESHI LA POLISI
Dar es Salaam: Mbunge wa Kawe kupitia chama cha Chadema, Halime Mdee ameripoti kituo cha Polisi Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuitikia wito wa Jeshi hilo aliotakiwa kufika leo Jumamosi Februari 23,2019.
Mdee kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika, “Nimepata wito wa kuitwa Polisi Oysterbay kwa mahojiano.”
“Mpaka sasa sababu ya wito ni nini. Ngoja tujongee.”
Halima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) alipofika polisi tulimpigia kujua kinachoendelea akasema. Nimepokelewa vizuri nipo hapa kwa RCO, Namsubiri nimsikilize.”
Sababu za kukamatwa kwa Mbunge huyo bado hazijafahamika lakini mchambuzi mmojo amesema kuwa Mdee amekuwa na mfululizo wa kauli za kuikosoa serekali juu ya uwamuzi wake wa korosha baada ya serekali kukaribisha wanunuzi wengine wa korosho kununu kwa bei nafuu, ''UNAJUA Bwana MagufuliJP anaweza ingia kwenye Guinness WORLD RECORD kwa kukurupuka!! Halafu yuko vyema sana kupotezea kimtindo na kujikausha kama ISSUE HAJAIFANYA yeye vile Wakulima (WANYONGE)na wafanyabiashara ndio WAMESHAUMIZWA vya kutosha #IndoPOWER " aliandika Mdee kupitia akauti yake twitter
kauli nyingine ya Mbunge huyo ni baada ya kuposti katuni moja inaonesha a korosha zimewekwa kwenye kiroba zingine zinaanza kuota ndipo mchangiaji mmoja akamuuliza ''Waheshimiwa simlitoa pongezi Sana huko mjengoni Mara tukasikia meza zikigongwa balaa,na wanyonge kule mikoa husika msiba akapost wamekesha wakipongeza. "kulikoni tena?" aliuliza mchangiaji mmoja, nae Mdee akamjibu''Ni bahati MBAYA HAMUONI Bunge. Tuliwaeleza BAYANA namna UAMUZI wa kukurupuka wa SERIKALI utakavyo gonga UKUTA!tukazomewa SANA kwamba tuna wivu na hatuwajali WANYONGE! SASA WANYONGE wanalia na kusaga meno,waliotengeneza TATIZO wame ‘MUTE’ kama hawapo nchini vile.