- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALI YA LISHE KWA WANAWAKE MIAKA 15-49 NI MBAYA SAVE THE CHILDREN WATOA ELIMU.
KINGALE: Imeelezwa kuwa hali ya lishe ya wanawake walio katika umri wa uzazi wa miaka 15- 49 bado ni mbaya pia tafiti zimebaini kati ya wanawake kumi wastani wa wawili wana utapiamlo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la 'Save ta Children' ambapo Kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Kingale Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa amesema lishe kwa wanawake wajawazito inachochea hatari ya kujifungua Watoto njiti , waliodumaa au Kuharibu Mimba.
Akiendelea kufafanua Mkurungezi huyo amesema hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi wakati au baada ya Kujifungua.
Aidha amesema Takwimu za hali ya ulishaji watoto wachanga na wadogo katika Mkoa huo takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri wa miaka miwili,wananyonyeshwa maziwa ya mama, idadi ya watoto wanaoanzishiwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi katika kipindi sahihi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 57.
"Idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 47.7, idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo cha ubora kiliishe ni asilimia 35.9 na idadi ta watoto wanaoanzishiwa vyakula cha nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 85.7,'' ameeleza.
Mbali na hayo alibanisha kuwa changamoto ya matumizi ya chumvi yenye madini joto, ni asilimia 81 Ndio wanatumia chumvi yenye madini joto la kutosha, mama mjamzito anatumia Chumvi siyo na madini joto, hivyo afya ya mtoto inaathiriwa sana kwani anaweza kuzaliwa akiwa na udumavu wa bongo au ulemavu wa viungo.
''Nitoe rai kwa wazazi na walezi kutafuta taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji unaofaa kutoka kwa mtoa huduma ya kiafya katika jamii, mtaalam wa afya kipindi cha ujauzito hili likienda sambamba na kuhudhuria Kliniki mapema pindi tu mama anapojigundua ni mjamzito,'' amesema Mkurugenzi huyo.
Pia amewataka akinababa kuwasindikiza wenza wao kliniki ili kuhakikisha kwamba mume/mwenza na familia wana taarifa kuhusu malengo ya unyonyshaji ili waweze kutoa msaada , pia aliwasisitiza kina mama wanaonyonyesha kuainisha msaada wa vitendo unaohitajika na kuomba msaada kutoka kwa mume/mwenza, familia na ndugu wengine ili kupata msaada.
Meneja wa Shirika la Save The Children kwa ufadhili wa Mfuko wa watu wa Marekani 'USAID' Mkoa wa Dodoma Benety Malima amewataka waajiri, wa mashirika na taasisi Binafsi kuhakikisha wanatenga chumba maalumu kwa ajili ya akinamama kuwanyonyesha watoto wao.
Amesema siku 1000 za lishe ya mtoto zinaanzia tumboni na nakuwasisitiza akinamama wajawazito kula vyakula vyenye lishe kabla na baada ya kujifungua.
Amesema kwa mujibu wa Takwimu za hali ya lishe kutoka Taaasisi ya Chakula na lishe kuwa katika Mikoa minne ambayo Shirika lao linafanyanao kazi hali ni mbaya ya kiliishe.
"Maeneo Makubwa ambayo sisi tumejikita ni Udumavu ambapo unaonekana kwa kiwango kikubwa sana, unyonyeshaji wa Mtoto," na kumtaka waziri kutoa masaa madili kwa mama ambaye anayonyesha ili kuweza kumnyosha mtoto wake.
Pia amewasisitiza akinababa kushirikiana nawamama katika suala zima la kunyonyesha na kuongeza kuwa wakati mwingine wa baba ni chanzo wa mama kutopata maziwa kutoka na ugomvi hivyo amewataka kuwapenda wake wao.