- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAKIMU AMUONYA ZITTO KWENYE KESI YA UCHOCHEZI
Dar es Salaam: Hakimu katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amemuonya mbunge huyo mara baada ya kushindiwa kufika mahakamani hapo kwa madai ya kuwa ni mgonjwa ambapo taarifa ya kuumwa kwake imetolewa na Shemeji wa Mbunge huyo.
taarifa za kuumwa kwake zimetolewa na Kasara ambaye ni shemeji yake Zitto, amedai amepigiwa simu asubuhi na dada yake (mke wa Zitto) na kupewa taarifa kuwa shemeji yake ni mgonjwa, hivyo aje mahakamani kutoa taarifa. "Nimepewa taarifa asubuhi na dada yangu kuwa shemeji yangu ni mgonjwa, ila sielewi anaumwa nini," amedai Kasara. Baada ya Kasara kueleza hayo, Hakimu Shaidi alimhoji shemeji yake Zitto, “kama shemeji yako anaumwa na hujui anaumwa nini na wala hujui yuko wapi? Sasa unakuja kutuambia mshtakiwa anaumwa bila maelezo ya kujitosheleza.
"Tusitafutane maneno hapa, mdhamini au ndugu unapaswa uje utoe taarifa iliyokamilika, kama mshtakiwa anaumwa, anaumwa nini? Yupo sehemu gani? Si unatoa taarifa ambazo hazijakamilika," amesema Hakimu Shaidi baada ya shemeji yake zitto kutoa maelezo ambayo hayakumridhisha.
Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu katika kesi ya uchochezi, inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya ugonjwa wa Zitto, zimetolewa leo Jumatatu Machi 11, 2019 na wakili wake, Steven Mwakibolwa, baada ya upande wa mashtaka kuieleza Mahakama hiyo kuwa hawamuoni mshtakiwa mahakamani hapo. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakamani hiyo, Huruma Shaidi, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa ushahidi, lakini mshtakiwa hayupo mahakamani hapo na upande wa mashtaka hawana taarifa zake.
Simon baada ya kueleza hayo, Wakili Mwakibolwa, anayemtetea Zitto amedai mteja wake ni mgonjwa na leo, ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake. "Nimepewa taarifa asubuhi hii kuwa Zitto ni mgonjwa, lakini amekuja shemeji yake mahakamani hapo kutoa taarifa hivyo, ataieleza mahakama juu ya afya ya Zitto," amedai Mwakibolwa.
Hakimu Shaidi amemtaka shemeji wa Zitto, kufuata taratibu zinazotakiwa, wakati anawasilisha taarifa zinazohusu mshtakiwa. "Unatakiwa kufuata taratibu za kutoa taarifa sahihi kama sheria zinavyotaka, kwa sababu hapa tukisema na sisi tukaze vyuma, vitakuwa vigumu zaidi," amesema Hakimu Shaidi na kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 9, 2019 itakapoendelea na ushahidi. Zitto alifikishwa Mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza, Novemba 2, 2018 kujibu mashtaka matatu ya uchochezi katika kesi ya jinai namba 327/2018. Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.