- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAKIMU AITISHIA SEREKALI KUMFUTIA KESI HALIMA MDEE
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Thomas Simba ameitishia serekali juu ya nia yake ya kuifuta kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee kutokana na upande wa mashtaka kukwamisha kesi hiyo Kufuatia shahidi kutofika mahakamani mara tatu mfululizo.
Hakimu Thomas Simba ametoa kauli hiyo mara baada ya Wakili wa Serikali, Silivia Mitato kudai wakili anayeendesha shauri hilo amepangiwa kazi nyingine hivyo anaiomba mahakama impe muda ili apitie jalada hilo
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema kumbukumbu zake zinaonyesha shahidi Abdull Chembea amefika mahakamani hapo zaidi ya mara tatu na hajawahi kutoa ushahidi.
"Hili shauri mimi nitalifuta kwa kuwa shauri hili lipo tangu mwaka 2017 kila nikija namuona huyu shahidi anakuja lakini hakuna kinachoendelea, naona upande wa mashitaka mnakwamisha shauri lisiendelee, nawapa sharti mtakapokuja awamu ijayo nataka shauri hili liendelee," amesema.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 28 na Septemba 4, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.
Hadi sasa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi akiwemo mkuu wa kituo cha polisi cha Urafiki, mrakibu wa Polisi (SP), Batseba Kasanga.
Mdee anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais magufuli, Mdee alisema kuwa “anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki”, kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.