Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:39 pm

NEWS: FREEMAN MBOWE "HATUNA HARAKA YA KUMPOKEA MEMBE"

Dar es salaam: Mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania(CHADEMA) Freeman Mbowe amesema chama chao hakina pupa ya kumpokea aliyekuwa Waziri wa Mambo ya njee Bernard Membe aliyetimuliwa na chama tawala CCM Mwishoni mwa mwezi wa pili.

Image result for freeman mbowe na membe

Amesema kuwa wao kama chama hawawezi kufanya maamuzi yeyote bila kufanya Tafiti na wao kama chama wanao uwezo wa kupokea wanachama kutoka vyama mbalimbali ilimradi afuate itikadi ya chama chao.

“Sisi hatufanyi maamuzi yetu bila tafiti, Chama chetu kinaweza kupokea Wanachama kutoka Vyama mbalimbali, inawezekana sana katika Siasa aliekuwa adui yako jana leo akawa mwenzako, tumepata faida na hasara kuchukua watu kutoka CCM, tumejifunza”. amesema MboweImage result for freeman mbowe na membe

Mbowe ambaye ni kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo leo Marchi 5, 2020 wakati akifanyiwa mahojiano na kipindi cha JAHAZI kinachorushwa na Redio ya Clouds Fm.

“Hatuna haraka ya kumpokea kada yoyote wa Chama cha Siasa, anapojitokeza mtu anataka kujiunga CHADEMA tunaweza mpokea na kumuweka ktk uangalizi, nisingependa kwenda kwenye mjadala wa Membe sababu ana haki ya kujiunga na CHADEMA akiona kinakidhi matamanio yake ya kiitikadi” amesema Mbowe

Mbowe amebainisha kuwa chama cha Chadema kimepata faida na Hasara kuchukuwa watu kutoka chama cha Mapinduzi

Membe alifukuzwa Mnamo Februari 28, 2020 baada ya kikao cha Kamati kuu cha CCM kukubaliana kwa pamoja

Membe alikuwa akikabiliwa na tuhuma za maadili pamoja na viongozi wengine waandamizi wengine wawili makatibu wakuu wa zamani Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, ambao wao hawajafukuzwa.

Bernard Membe

Makamba amesamehewa, huku Kinana akionywa kwa karipio.

Membe, Makamba na Kinana walipelekwa katika kamati ya maadili ya CCM mwezi Disemba mwaka jana, na taarifa ya chama hicho ilidai kuwa viongozi hao pamoja na makada wengine watatu ambao walisamehewa walikidhalilisha chama mbele ya Umma.

Makada ambao walitangazwa kusamehewa ni January Makamba, Nape Nnauye na Wlliam Ngeleja ambao wote walimuomba radhi mwenyekiti wa CCM na rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Baadhi ya mazungumzo ya simu ya wanachama hao sita wa CCM yalivujishwa kwenye mitandao nchini Tanzania wakizungumzia masuala mbalimbali kukihusu chama na mwenyekiti wake.

Sehemu ya mazungumzo yaliyovuja ya Mzee Yusuf Makamba na Kinana ni pamoja na kuandaa taarifa ya malalamiko dhidi ya 'mawanaharakati' Cyprian Musiba ambaye wanamtuhumu kwa 'kuwadhalilisha' bila kuchukuliwa hatua yoyote na kuhoji analindwa na nani.

Membe na tuhuma za kutaka kumhujumu Magufuli

Kwa upande wa Membe, licha ya kusikika kwenye mazungumzo hayo yalivuja, amekuwa pia akituhumiwa na baadhi ya wanchama wa chama hicho kuwa najipanga 'kumhujumu' Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Membe amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na mipango ya kutaka kugombea tiketi ya urais kupitia CCM mwaka huu, hatua ambayo baadhi wanaitafsiri kama usaliti.

Japo katiba ya CCM inaruhusu hilo, imekuwa ni ada ya chama kumuachia rais aliye madarakani kupita bila kupingwa kwa awamu ya pili ya urais.

Baadhi ya watu tayari wanatafsiri kufukuzwa kwa Membe ni kutokana na kuhusishwa huko na mipango ya Urais.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kwa kupitia mtandao wake wa Twitter amepeperusha maoni yake na kuhusisha urais na kufukuzwa uanachama kwa Membe.