Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:44 am

NEWS: FATMA KARUME KUMFUNGULIA KESI JAJI KIONGOZI JUMATATU HII.

Dar es Salaam: Rais wa chama cha wanasheria Tanzania(TLS) Fatma Karume anatarijia kumfungulia Mashitaka Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Dk Eliezer Feleshi, kwa kosa la kukataa kuisajili kesi yao ya kikatiba ya kupinga Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhojiwa na Kamati ya Kinga na Maadili ya Bunge.


Bi Karume ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Zamani wa Zanzibar Amani Abeid Karume alitangaza nia hiyo jana Januari 19, 2019 baada ya usajili wa kesi hiyo kushindikana kwa siku ya tano mfululizo.

Akizungumza na muakilishi Media kuhusu hatua wapofikia juu ya usajili wa kesi hiyo, Karume alisema juhudi za kusajili kesi hiyo zimeshindikana na sasa anaandaa kesi dhidi ya Jaji Kiongozi ambayo anatarajia kuifungua Jumatatu.

“Natarajia kuifungua hiyo kesi Jumatatu na kama wataikataa kuisajili hii, basi nitaipeleka Mahakama ya Afrika Mashariki,” alisema.

Tarehe 16 Januari 2019 Mbunge wa Kigoma Ujiji pamoja na wabunge wengine wanne waliwasilisha kesi katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga CAG kwenda kuhojiwa na kamati ya Bunge, lakini baada ya kufika kwa msajili wa kesi Dk Eliezer Feleshi, aligoma kuipokea kesi hiyo na kutokomea kusiko julikana.

"Kuna mambo nikikumbuka nacheka kwa hasira sana. Leo (Januari 16 ) msajili wa Mahakama Kuu ametukimbia ili tukirudisha shauri tusimkute na akaacha maagizo kwa makarani wasipokee kesi. Yani kafunga Ofisi na kwenda kujificha! Nilihisi nywele zimesimama kwa hasira. Hali ya fatma karume usiseme" alisema Zitto Kabwe