- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: FATMA KARUME AVULIWA UWAKILI, MWENYEWE ASEMA HAELEWI SABABU
Leo Septemba 20, 2019 Jaji Kiongozi Elinezer Feleshi, ametangaza kumvua uwakili wa Tanzania Bara Wakili Fatma Karume, kwa kile alichokieleza anaishambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Mwenyewe Fatma Karume amesema hajui sababu iliyomfanya mpaka asimamishwe uwakili Tanzania Bara.
" Leo Feleshi J kanivua uwakili wakati nilikuwa sipo Mahakamani. Hajanipa notice ya malalamiko dhidi yangu na wala kunipa muda wa kujitetea. Pengine Siasa na si Mahakama ndio italeta mabadiliko" ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter
Akizungumza na EATV/EA Radio Digital, Fatma Karume, amesema ameshangazwa na taarifa hizo, kutokana na maamuzi hayo kufanyika bila yeye kuwepo mahakamani na kukosa nafasi ya kujitetea.
"Ni kweli Jaji Feleshi amenipiga 'stop' na wala sijui nini kinafuata kwa sababu mimi sikuwepo mahakamani, na kanipiga stop wala hajaniambia kosa langu ni nini ?'', amesema Fatma Karume.
"Kuhusu hatua zinazofuata mimi sijui nahitaji kutuliza akili yangu, nahitaji kujiuliza na kufikiria kama nahitaji kuendelea kuwa Wakili Tanzania Bara, lakini si lazima niseme sasa hivi nitafanya nini, lakini kwa sasa bado ni mimi ni Wakili Zanzibar." amesema Wakili Fatma Karume