- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: FAMILIA YA TITO MAGOTI YASHINDWA KULALA
Familia ya Ofisa wa Elimu kwa Umma wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu LHRC, Bw. TITO MAGOTI imesema kitendo cha Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kumshikilia ndugu yao na hadi Leo kushindwa kuwaonyesha kituo alipo kinawapa hofu kubwa.
Kaka wa Ofisi aliyetoweka Ijumaa ya December 20 mwaka huu EDWIN MAGOTI ameongea na Clouds Media kuwa walipopata taarifa kuwa ndugu yao anashikiliwa na Jeshi hilo walipata ahueni, lakini kitendo cha jeshi hilo kutosema wamemuhifadhi wapi na wanamshikilia kwa kosa gani kinawapa wasiwasi mkubwa.
EDWIN anasema tangu kutokea kwa tukio hilo hakuna ndugu anayekula na kulala kwa raha katika familia yao, huku akiliomba jeshi la Polisi kueleza ni kosa gani alilotenda ndugu yao ili wamuwekee dhamana.