Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:31 am

NEWS: FAMILIA YA LISSU KUFUNGUA KESI KUDAI GHARAMA ZA MATIBABU

Kaka wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Wakili Alute Mughwai amesema wao kama familia wanania ya kufungua mashtaka kudai haki za ndugu yao, ikiwemo gharama za matibabu aliyostahiki kupewa na Bunge la Tanzania

Image result for Alute Mughwai​

Wakili Mughwai ameyaongea hayo jana wakati akifanyiwa mahojiano na gazeti la Mtanzania jijini Arusha, alisema Lissu anatarajiwa kurejea nchini Septemba 7 mwaka huu.

Wakili Mughwai alisema Lissu ataenda kuonana na madaktari wake Agosti 20 kufanyiwa vipimo mara ya mwisho kabla kupewa ruhusa ya kuondoka hospitalini.

Alisema maandalizi ya ujio wake yanaendelea na kuwa taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Image result for Alute Mughwai​

Wakili Mughwai alisema kwamba Lissu alishasema atakwenda mahakamani kudai haki zake, kwamba amekuwa akilalamika hakutendewa haki na ofisi ya Bunge ya kutokutibiwa kwa gharama ya mhimili huo, kama ambavyo alikuwa anastahili, pamoja na kulipwa posho akiwa hospitalini.

“Nia yake ya kwenda mahakamani juu ya jambo hili bado ipo, na akirudi pamoja na mambo mengine atachukua hatua hiyo kufungua shauri mahakamani ili mahakama iweze kuamua kama madai yake kutibiwa kwa gharama za Bunge ni halali au hapana.

“Aidha kwa kupitia mahakamani, atauliza ofisi ya Bunge ni kwanini mpaka sasa hivi uongozi wa Bunge haujaanzisha bima kwa ajili ya matibabu ya wabunge nje ya nchi pale inapohitajika kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa shughuli za Bunge ya mwaka 2008, sura ya 115 ambapo kifungu cha 24 cha sheria hiyo kinasema Bunge litaweka bima mahsusi kwa ajili ya mbunge.

“Mwenza wake au watoto wasiozidi wanne wenye umri chini ya miaka 18 haki ya kupata matibabu ndani na nje ya nchi, ila utaratibu wa sasa hivi wabunge wana bima ya kutibiwa ndani ya nchi, lakini hakuna bima yao ya kutibiwa kama itahitajika nje ya nchi, na ndiyo takwa la kisheria na wabunge wanaohitaji kutibiwa nje ya nchi inabidi wategemee huruma za watu wengine,” alisema Mughwai.

Alisema suala la pili atakalofuatilia Lissu ambaye alikuwa ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ni kuweka msukumo wa tukio la Septemba 7, 2017 la shambulio la kujaribu kumuua akiwa nje ya makazi yake jijini Dodoma, ili uchunguzi wa tukio hilo ukamilike na watakaobainika kuhusika wafikishwe kwenye vyombo vya dola.