Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:42 pm

NEWS: ESTONIA YAWA NCHI YA KWANZA KUTOA USAFIRI WA BURE KWA WANANCHI

Image result for estonia public transport

Nchi ya Estonia yaweka rekodi kuwa nchi ya kwanza kuwa na Usafi wa Bure, hii ni baada ya serekali ya nchi hiyo kuja na wazo la kuwa na usafiri bure wa Umma, Wazo hili la Estonia lilikuja mara baada ya kutokea kwa Mgogoro wa kiuchumi (financial crisis) wa nchi hiyo ulioikumba mwaka 2008.

Hapo awali Serekali ya Estonia ilikuwa ikiwalipia wananchi masikini gharama za tiketi za kusafiria kwenye usafiri wa umma kwa asilimia 70%, lakini bado kiasi cha asilimia 30% kilikuwa kikionekana kuwa ni ghali mno kwa wananchi hao kuumudu.

Image result for estonia public transport

Magari hayo yanawasili kwenye vituo kwa muda muafaka na abiria wote wanapata siti za kukalia, kwenye miji mingi ya Estonia walikuwa watu wanakata tiketi kuingia lakini mji wa Tallinn mwaka 2013 ulikuwa hauhitajiki abiria kukata tiketi na ukaifanya kuwa mji wa kwanza duniani kuwa na usafiri wa bure.

Na kwasasa mabasi ya Usafiri wa Bure yanapatikana katika miji 11 kati ya 15 kwenye nchi hiyo sawa na asilimia 73% ya miji yoote.