Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:19 pm

NEWS: ESTER BULAYA AMRIDHI TUNDU LISSU , SASA NI MNADHIMU MKUU BUNGENI

Dodoma. Bunge la Tanzania leo Januari 28, 2020 limemtangaza Mbunge wa Bunda (Chadema), Ester Bulaya kuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni akirithi mikoba iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Singinda Mashariki Tundu Lissu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Spika wa Bunge hilo Job Ndugai akibainisha kuwa amepokea jina hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe.

Bulaya anachukua nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyevuliwa ubunge kwa madai ya kutoonekana bungeni bila taarifa yoyote. Kabla ya uteuzi huo wa Bulaya, mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alikuwa anakaimu nafasi hiyo. Selasini alijiuzulu wiki iliyopita

"Naahidi kuhakikisha natetea na kupigania haki bila chembe ya uoga, maslahi ya kambi rasmi ya upinzani na niko tayari ku-sacrifice kwa sababu maoni mengi ya kambi rasmi yanagusa maoni ya wananchi" Mhe. Ester Amos Bulaya

Mbali na kumtangaza Bulaya, Spika Ndugai amempongeza Mbowe kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa Chadema na John Mnyika kuwa katibu mkuu wa chama hicho.