- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ERICK KABENDERA AHUKUMIWA KULIPA MILIONI 297
Dar es Salaam. Mwandishi wa habari, za uchunguzi nchini Tanzania Erick Kabendera amehukumiwa na Mahakama ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa fidia ya Sh172 milioni baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi na kulipa faini ya Sh250,000 kwa kosa hilo la kukwepa kodi.
Wakati huo huo Katika shtaka la kutakatisha fedha, mahakama imemhukumu Kabendera kulipa faini ya Sh 100 milioni na tayari ameshailipa.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Februari 24, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya mshtakiwa kukiri mashtaka yake kwa njia ya majadiliano na Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Tanzania (DPP).
Katika mashtaka hayo Kabendera alikuwa akituhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania.
Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.
Kabendera anadaiwa kuyatekeleza makosa hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani leo.