- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ELIMU YA TAWA YAONGEZA TEMBO
DODOMA: MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyama pori (TAWA) imeeleza kuwa kwa sasa hali ya ujangili wa wanyama poli umepungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha tembo kuongezeka katika hifadhi mbalimbali za wanyama pori.
Kupungua kwa ujangili na kuongezeka kwa tembo kunaelezwa kuwa kunatokana na elimu ambayo Mamlaka hiyo imetoa kwa jamii ambayo inazunguka maeneo ya hifadhi ya wanyama sambamba na kuimarisha vikosi vya ulinzi kwa wanyama poli.
Hayo yameelezwa na Afisa habari na Mahusiano wa Mamlaka hiyo Twaha Twaibu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo na Mifugo ambayo yanafanyika katika viwanja vya Nane Nane kitanda Kata ya Nzuguni Manispaa ya Dodoma mjini hapa.
Twahibu amesema katika hatua ya kutoa elimu ya utunzaji wa maeneo ya wanyama poli pia wameweza kutoa elimu pana kwa jamii jinsi ya kuweza kukabiliana na wanyama ambao wanaharibu mazao kama vile tembo bila kuwahua kwa kutumia siraha wala kuwadhuru.
Pia amesema elimu hiyo imeweza kuwaongezea kipato wananchi ambao ni wakulima wanaohisi pembeni mwa mapori ya hifadhi kwa kuwataka walime mazao ambayo hayaliwi na Tembo kama vile ufuta , kufuta nyuki pamoja na kuweka kamba za mafuta machafu katika mipaka ya mashamba yao na kufunga kamba zenye pilipili.
Akizungumzia kuongezeka kwa tembo amesema dalili kubwa licha ya kutokuwepo kwa takwimu kwa sasa lakini viashiria vinaonesha kuzagaa kwa tembo kutoka eneo moja kwenda eneo linguine na mfano ni siku za karibuni ambapo tembo walionekana wakizagaa katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
“Tumeboresha zaidi mazingira ya maonesho ya nane nane,kwa sasa tumeleta wanyama tofauti na miaka mingine kwa sasa tumeleta,Mamba,Tusi ambao wanaonekana zaidi Ikulu, Nyati, Ndege aina aina ya taji Korongo wanaotumika katika nembo ya bendera ya Nchini Uganga”alieleza Twahibu.
Kutokana na hilo Twaibu amewataka wananchi wa maeneo mbalimbali kutembelea banda la wanyamapoli hai wanaooneshwa katika maeneo hayo ili kuweza kujionea wanyama watofauti ambao ni fahari kwa utalii wa ndani.
Hata hivyo Twaibu akizungumza na waandishi wa habari amesema kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na TAWA kama wasimamizi wakuu wa pori la Akiba Selou (Urithi wa Dunia) wanaunga mkono maamuzi ya serikali ya awamu ya tano kupitia rais Dk.John Magufuli, kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji kwenye poli la Akiba la Selous ambao ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya Megawati 2,100.