- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DR BASHIRU AUSIFIA MUSWADA VYAMA VYA SIASA, ATAKA KUTOBADILISHWA
Dodoma: Katibu Mkuu wa chama tawala CCM, Dk Bashiru Ali, amesema muswada wa sheria wa vyama vya siasa ni mzuri kwahiyo asingependekeza utolewe hata koma moja.
Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 17, 2019 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wanachama wa CCM wa mkoa wa Dodoma waliokusanyika kutoa maoni yao kuhusu muswada huo.
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa White House ambao ulifurika wana CCM, Dk Bashiru alisema kuna wababaishaji ambao wanataka kuyumbisha nchi kwa maslahi yao binafsi. "Kuna mbabaishaji mmoja sitaki kumtaja jina alikimbia chama fulani akisema wanatumia vibaya ruzuku lakini leo tunaleta muswada wa kudhibiti ruzuku kwa vyama anapinga tena, huyu ni mtayarishaji," amesema Dk Bashiru.
Dk Bashiru amewataka wana CCM kuujadili muswada kwa nia njema kwani unakwenda kuimarisha siasa za Tanzania na kuweka imara vyama vya siasa na vinavyotaka kuanzishwa. "Lakini msiwe na wasiwasi, mashine zimetegwa tayari kinachosubiriwa ni kuanza kazi tu wala si kusubiri, tuko imara kisiasa na chama chenu kiko imara kuliko wakati mwingine," amesema. Kiongozi huyo amewataka viongozi wa CCM kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani