Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:30 am

NEWS: DR BASHIRU AMSIFU LUSINDE KUWAJIA JUU KINANA NA NAPE NA MAKAMBA

Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amempongeza mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde kwa kutoa kauli ya kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuagiza polisi kumhoji Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana juu ya tuhuma zinazowakabili juu ya waraka na kuvuja kwa sauti.

Image result for dr bashiru ally

"Fanyeni kazi ya uenezi, nampongeza Lusinde alipoona hali ya uwanja si nzuri alifungua mlango wa chooni akapuliza pafyumu, akatokea mlango wa nyuma akapaa zake China, safi sana," amesema Dk Bashiru.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 23, 2019 mkoani Dodoma katika mkutano na wanachama wa chama hicho mkoani humo.

Jumamosi Julai 20, 2019 Lusinde, ambaye amepachikwa jina la “Kibajaj” alizungumza na waandishi wa habari kuhusu sauti zilizosambaa mitandaoni zikidaiwa kuwa ni za Nape, ambaye ni mbunge wa Mtama na Kinana, aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, zikimtaja Rais John Magufuli katika masuala mbalimbali.

Related image

Mbunge huyo alitaka wawili hao kuhojiwa na polisi kuhusu sauti hizo, kuahidi atakaporejea katika safari yake ya China atazungumza kuhusu sauti zinazodaiwa kuwa za makada mbalimbali wa CCM.

Si Nape wala Kinana, ambaye hivi karibuni aliandika waraka kwa baraza la ushauri la viongozi wastaafu kulalamikia kuchafuliwa, aliyejitokeza kuzungumzia sauti hizo, wala hakuna waliothibitisha kuwa sauti hizo ni za makada hao, lakini Lusinde anataka wawili hao wahojiwe.

Amewasifu viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma kwa kutoa tamko la kukemea barua inayoandikwa na Kinana na katibu mkuu mwingine wa zamani wa chama hicho, Yusuf Makamba kwenda kwa katibu wa baraza la ushauri la viongozi wakuu wastaafu wa chama hicho wakilalamika kudhalilishwa kwa