Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:34 pm

NEWS: DPP AKATA RUFAA WANAHABARI KUHUDHURIA MAHAKAMANI KESI ZA UGAIDI

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amekata rufaa Mahakama Kuu akipinga wananchi na waandishi wa habari kuingia kusikiliza na kuripoti kesi ya ugaidi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmedi na wenzake 22.

DPP amefikia uamuzi huo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde Septemba 5, 2019 kutoa uamuzi akiruhusu waandishi wa habari kuingia katika kesi hiyo wakati inaendelea.