- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DOKTA MBARONI KWA KUMUUA MPENZI WAKE KWA NYUNDO
Jeshi la polisi Mkoani Kigoma linamshikilia daktari wa Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) Albert Rugai (65) kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa nyundo ya msumari na yeye kutaka kujiua baada ya kumua mpenzi wake huyo.
Akizungumzia tukio hilo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno amesema kuwa chanzo cha tukio hilo lililotokea Jumapili, Januari 12 mwaka huu ni wivu wa mapenzi baina yao.
Kamanda Otieno amesema kuwa mtuhumiwa huyo alimpiga kwa nyundo kichwani mara mbili mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Esther Kondo (42) hali iliyomsababishia majeraha makubwa kichwani, akavuja damu na ubongo kutoka nje.
Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kujiua kwa kunywa sumu, jaribio lililoshindikana na sasa anapatiwa matibabu na atakapopona atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili, ameongeza kamanda huyo huku akiwataka watu kutokujichukulia sheria mkononi. "Ninawashauri wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kama unaona mpenzi wako ana shida achana naye na utafute mwingine usijitafutie matatizo kwani huyu mzee na umri wake anaenda kufia jela." Kwa sasa mtuhumiwa huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kibondo ambapo pia ndipo ulipo mwili wa aliyekuwa mpenzi wake.