- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DODOMA TISHIO KWA MIMBA ZA UTOTONI
DODOMA: KATIKA kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika bado suala la mimba za utotoni limeonekana kuwa ni tatizo ambapo Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni.
Aidha asilimia 51 ya wasichana wenye umri wa miaka 20 hadi 22 wameolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalum FATUMA TAWFIQ wakati alipokuwa akizindua maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambapo amesema, kutokana na takwimu hizo kuwa juu hivyo ni vyema wakazi wa Mkoa wa Dodoma kulipinga suala hilo.
Mbunge huyo amewataka watoto na wazazi kutumia muda wao katika kuzungumza nao juu ya athari za mimba hasa kujiingiza katika mahusiano kwenye umri mdogo
Hata hivyo baadhi ya wananchi ili kuweza kujua wao wana maoni ganikuhusu siku ya mtoto wa Afika na nini maoni yao ambapo walikuwa na haya ya kusema
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila tarehe 16 ya mwezi Juni ambapo Kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma Katika wilaya ya Chamwino kata ya Haneti na kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni maendeleo endelevu 2030 imarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto.