- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Dkt. Ndugulile atembelea MOI,akagua maendeleo ya chumba cha tiba mtandao.
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea Taasisi ya Tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI)kukagua maendeleo ya chumba maalum cha Tiba mtandao ambacho kinatarajia kukamilika na kufanya kazi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Awali akiwa kwenye taasisi hiyo ya MOI, Dkt. Ndugulile aliweza kupokea maendeleo ya ukamilishwaji wa chumba hicho cha tiba mtandao ambapo pia aliwataka kuhakikisha wanasimamia vizuri uendeshaji wake kwani utasaidia Taifa kutoa huduma za kibingwa sehemu kubwa zaidi hapa nchini.
Aidha, Dkt. Ndugulile amewataka kukamilisha hatua zote za chumba hicho na kitakapokamilika uzinduzi ufanyike kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Respicious Boniface amesema kuwa, chumba hicho kinategemea kukamilika na kuanza kufanya kazi mwezi Juni mwaka huu na kitakapokamilika kitasaidia matibabu kwa kwa njia ya mtandao nchi nzima.
“Chumba cha Tiba mtandao hapa MOI kitakapokamilika hospitali zote kubwa za rufaa za mikoa na zingine za Rufaa, zitatuma picha hapa na watalaam wa MOI wanatoa majibu na kurudisha tiba kule na kutoa ushauri wa jinsi wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wakiwa hukohuko” alieleza Dkt. Boniface.
Chumba hicho cha tiba mtandao kinatarajiwa kuwepo kwenye jengo jipya la MOI ambapo tayari timu ya watalaam wanaendelea na taratibu za kukamilisha uendeshaji wake.
MOI ni miongoni mwa Taasisi za tiba zenye kutoa huduma za kibingwa huku ikiwa na Madaktari wabobezi kwenye tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.