- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DKT MAGUFULI AJIVUNIA MFANIKIO YA MUUNGANO, AAPA KUULINDA
Dodoma: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama nchini,Dkt.John Magufuli leo ameongoza mamia ya watanzania katika maadhimisho ya sherehe ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .
Rais Dkt . Magufuli amesema mafanikio yaliyopatikana kutokana na Muungano yamefanikishwa kutokana na juhudi za viongozi wa taifa na waasisi wa Muungano huo.
Rais magufuli pia amewataka watanzania kudumisha amani iliyopo nchini na kwamba asitokee yoyote wa kuvunja amani.
Sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimefanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri ikiwa ni mara ya kwanza kwa sherehe hizo kufanyika mkoani Dodoma.
Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uliundwa tarehe 26 Aprili 1964,ambapo muungano huo ulizinduliwa rasmi na Mwalimu Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na Sheikh Abeid Aman Karume, Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Karimjee Hall, Dar es Salaam.