- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DKT BASHIRU AWAELEZA VIJANA KUWA DIGRII SIO PESA
Dkt. Bashiru amesema, yeye ni Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa, lakini hakuna magulio asiyoyafahamu wilayani Bukoba, kwa kuwa alipokuwa anasoma na baada ya kuhitimu masomo yake, kazi kubwa aliyokuwa akiifanya bila uwoga ni uchuuzi kwenye magulio kazi ambazo vijana wengi wakiwa na shahada kichwani hawawezi kuzifanya.
Dkt. Bashiru ameyasema hayo, juzi Desemba 29, 2019 alipokuwa akitoa salamu za Chama wilayani Muleba kata ya Mayondwe katika shughuli ya dua iliyojumuisha maombi mbalimbali pamoja na kuiombea amani nchi yetu. “Vijana bila kuchapa kazi maisha yatabana, na vyuma vitabana kwelikweli, mimi ni Katibu Mkuu kwa sasa hakuna magulio nisiyoyafahamu hapa Bukoba na Muleba kwa kiasi, wakati nasoma na baada ya kuhitimu masomo kazi kubwa niliyoifanya kwa muda mrefu ni uchuuzi kwenye magulio kazi ambayo vijana wengi wakiwa na shahada kichwani hawapendi kuzifanya.’’ Bashiru ameeleza
Ameongeza kuwa, ukiwa na elimu ya shahada kichwani hiyo sio pesa, ila maarifa yako ndio yatatengeneza pesa akimtolea mfano Bw. Jafari Swalehe waliosoma naye darasa moja shule ya msingi Katerero na kuishia darasa la saba mkazi wa Bukoba vijijini ambaye kwa sasa ni mkulima mkubwa wa mbogamboga na matunda wilayani hapo.
Wakati huo huo, Dkt. Bashiru ameeleza wazi kuwa, CCM inajukumu la kutunga Sera wezeshi ili kundi kubwa la vijana waweze kupata mazingira mazuri ya fursa mbalimbali zikiwemo biashara, kilimo na viwanda, ambalo wameendelea kulifanya na katika Sera na Ilani ijayo suala hili litapewa uzito wa pekee ili kuwezesha kundi kubwa la vijana kupata na kumudu fursa za kimaendeleo.
Aidha, Dkt. Bashiru katika salamu hizo amehimiza upendo miongoni mwa wanafamilia na jamii kwa ujumla, ambapo ameeleza kuwa, maisha yetu ya upendo na undugu hutegemea maisha yetu ya kila siku, maisha ya upendo hutengenezwa katika ndoa, shule, siasa, biashara na maeneo mengine.