Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:38 pm

NEWS: DK.MASHINJE ALIKOROMEA BUNGE

DODOMA: KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Vicent Mashinji,amelituhumu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuvunja Katiba ya nchi na kuomba fedha kwa Serikali bila kufuata utaratibu,

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mashinji amesema, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila ameandika barua kwenda kwa Waziri Mkuu na nyingine kwa Katibu Mkuu Hazina akiomba fedha ajili ya amatumizi mbalimbali.

Serikali imeshatoa Shilingi bilioni saba kwa ajili ya Bunge, lakini huko nyuma tumeshuhudia ukiukwaji wa Katiba baada ya serikali kununua ndege, kujenzi wa kiwanda cha ndege Chato bila kufuata utaratibu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara yetu ya 73 inasema kuwa wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa katiba hii na watalipwa mshahara, posho, na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

“Tatizo hapa siyo kupeleka pesa bungeni, tatizo ni kufuata utaratibu, Bunge ndilo linalopitisha bajeti iweje leo linaomba omba? Bunge limevunja ibara ya 137/3A na B kwa kuomba fedha za ziada nje ya bajeti yake iliyoidhinishwa na Bunge bila kufuata utaratibu wa kuipitisha bungeni,” ameongeza Mashinji.

Mwaka wa Fedha 2016/17 wabunge wamekuwa wakiondoka bungeni bila kulipwa stahiki zao moja ya sababu iliyosababisha Dk Kashilila kuandika barua ya kuomba pesa kwa Serikali.