- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DK BASHIRU ANASEMA LISSU ANAUGUA UGOJWA WA 'KUDEKA'
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), anaumwa ugonjwa wa Kudeka au (DEKO) na kwa maana hiyo amemuomba Rais Dk. John Magufuli aanze hatua za kuutibu ugonjwa huo kwa sababu ni Ugojwa hatiri na unapaswa kuogopwa zaidi ya Ukimwi
Kauli ya Bashiru aliitoa jumamosi wilayani Kilosa mkoani Morogoro, katika ziara yake ya kikazi ikiwa ni sehemu ya maadhimino ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM, ambapo Lissu amekuwa akisema uongo katika nchi za Ulaya huku akiota siku moja atakuwa Rais wa Tanzania.
Wakati mtendaji huo wa juu wa CCM akiyasema hayo, Lissu amekuwa akiendeleas na ziara yake katika nchi za Ulaya ambapo kwa sasa yupo nchini Marekani akieleza kile alichodai hali ya demokrasia nchini na kupigwa kwake risasi.
Kutokana na hali hiyo Dk. Bashiru, alisema kuwa dalili za ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.
“Ila shukrani ya Punda ni mateke. Namuomba Rais wetu (Dk. John Magufuli) aanze kutibu ugonjwa wa deko unasomesha watu wanazunguka kutukana nchi yao na Rais wao kisa ugonjwa wa deko.
“Yupo msomi mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua ugonjwa wa deko, anadeka hajui jembe kwa maisha yake, hajui mpunga unalimwaje wala samaki wanavuliwaje.
“Hajapanda bodaboda muda mrefu na watoto wake hawasomi shule hizi anazunguka dunia nzima kutuchafua. Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini tumewaamini tumewapa dhamana ila ukiwatembelea ofisini wanadeka, mara nyingine hawapo, wanajipendelea wao,” alisema Dk. Bashiru