- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DIWANI WA CCM DODOMA MBARONI
Dodoma: Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Diwani wa kata ya Makole (CCM), jijini Dodoma Habel Shauri kwa tuhuma ambazo hazikuwekwa wazi na Jeshi hilo, lakini zikihusha hasa na migogoro ya Ardhi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amedhibitisha kukamatwa kwa Diwani huyo lakini hakuwa tayari kutoa sababu za kumshikilia Diwani nhuyo alisema “Ni kweli tumemkamata tunachunguza. Hatuwezi kulizungumza kwenye vyombo vya habari tutakujulisha siku tutakayompeleka mahakamani na ndipo utakapojua kilichosababisha akamatwe.
” Alipoulizwa ni siku ya ngapi tangu wamkamte diwani huyo Muroto alisema “Hatuwezi kusema ni siku ya ngapi kubwa uchunguzi unaendelea.” Wakati Kamanda Muroto akisema sababu za kumkamata zitawekwa wazi atakapofikishwa mahakamani, Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema diwani huyo anashikiliwa kuhusiana na masuala ya ardhi. Hata hivyo, hakutaka kuingia undani wa suala hilo akisema jeshi la polisi lipo kwenye uchunguzi.
“Ni kweli amekamatwa kwa sababu ya masuala ya ardhi na bado suala hilo chini ya upelelezi. Ni mapema kusema muda tangu akamatwe, lakini nafikiri ni siku ya tano kama sio ya sita,” alisema Profesa Mwamfupe.