- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DIWANI ACT WAZALENDO ATUPWA MIEZI 5 JELA
Kigoma: Mahakama ya mwanzo Mwandiga Kigoma imemuhukumu Diwani wa Mwanga Kaskazini kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumshambulia askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Akitoa hukumu hiyo leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga, Hakimu Mkazi, Florence Ikolongo amesema Baba Levo alimshambulia askari F.8350 PC Msafiri Mponela.
Hakimu Ikolongo amesema kifungo hicho ni bila faini. Karani wa mahakama hiyo, Jackson Mrefu amesema Baba Levo ametiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002.
Kufuatia hukumu hiyo ya kesi namba 52/2019 iliyomtia hatiani Baba Levo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, katibu wa ACT mkoani Kigoma, Juma Ramadhani amesema chama hicho kinafuatilia na kitatoa tamko.
"Kama chama tumepokea taarifa ya diwani wetu kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano na tumeambiwa kwamba alichukuliwa na gari kupelekwa gerezani, tutatoa taarifa rasmi ya chama leo mchana na jamii itajua msimamo wetu,β amesema Ramadhani.
Tukio la kumshambulia askari lilitokea July 15 majira ya saa moja usiku katika eneo la kwabela ambapo baba Levo alimshambulia askari wa barabarani anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alilazimisha kupita kwa pikipiki eneo la watembea kwa miguu wakati askari huyo ameshawaruhusu watembea kwa miguu kuvuka,baada ya hapo baba levo alimua kumshambulia askari huyo. Diwani wa kata ya Kigoma mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Hussein Kaliyango amesema kuwa tayari wameshaanza mchakato wa kukata rufaa ili haki ya baba Levo ipatikane.
"Tunashukuru maamuzi ya mahakama tunakata rufaa leo hii tunaingiza rufaa tunaamini haki ya Baba levo itapatikana, Niwatoe hofu wananchi wa kata ya mwanga kaskazini kuwa tunakata rufaa tunaimani mahakama itatenda haki"alisema Diwani huyo Alisema Baba levo ni mtetezi wa Bodaboda,Bajaji na wanyonge wajasiliamali katika Manispaa ya Kigoma amewapambania vya kutosha leo amepatikana na hatia kwa nia ya kuwatetea wananchi wa mji mzima ndio alivyozaliwa baba levo hii ndio safari ya kuwa mwanasiasa mkubwa nchini.