Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:18 pm

NEWS: DIAMOND ATANGAZA KIAMA CHA BURUDANI TAMASHA LA WASAFI

Nyota wa muziki wa Bongofleva na Bosi wa label ya WCB Nasib Abdul maarufu kama Diamond platnumz amewataka wasanii wenzake kutumia Sanaa yao kuongeza pato la taifa huku akimpigia chepeo msanii aliyeihama label hiyo Harmonize na kusema kuwa Harmonize ni mtoto wa Wasafi hivyo ushiriki wake katika tamasha hilo hauna pingamizi lolote.

"Harmonize ni zao la Wasafi na atabaki kuwa Wasafi, hivyo hata kushiriki kwenye tamasha ni haki yake,” amesema Diamond.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam wakati akitangaza rasmi ujio wa Tamasha la wasafi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam amesema kwa mwaka huu imekua neema kwa wasanii wasanaa mbalimbali kupewa nafasi na Waziri wa utalii Hamisi kigangwala kutembelea vivutio vilivopo nchini hasa mlima Kilimanjaro nakujifunza vingi zaidi.

" Tumeanza kupanda mlima Kilimanjaro lakini vingine vingi vitafata lengo likiwa ni kuutangaza utalii wetu kwa nchi za nje ili kujua vitu tulivobarikiwa sisi Kama watanzania,"

Hata hivyo platnum ameeleza ujio huo wa Tamasha utakua ni mara ya Kwanza kwake kutumbuiza Dar es Salaam kwani hakuweza kufanya hivyo kutokana na kukosa kibali kwa mwaka Jana kutokana na utovu wa nidhamu uliofanyika .

"Niliweza kutumbuiza uwanja wa Taifa katika Tamasha la jamaa lililoandaliwa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ,Basi pale niligusa gusa tu balaa lenyewe mashabiki na wapenzi wa lebo ya wasafi (WCB) wajitokeze novemba 9 mwaka huu katika viwanja vya posta jijini Dar es salaam,"

Pia amegusia swala la vijana kupima afya zao nidhahiri wamekua wakipata ushirikiano wakutosha kutoka Taasisi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi (TACAIDS) na kupewa fursa Kila mkoa kuungana nao na kutoa elimu juu ya kujikinga na kuepuka maambukizi ya ukimwi.

Hata hivyo amefafanua kuwa Wana lengo la kuwa tofauti katika Tamasha la mwaka huu hasa la Dar es salaam na mashabiki wategemee uwepo wa wasanii wengine wengi kutoka nje ya nchi lengo ni kupata burudani kabambe.

Diamond amesema mbali na Harmonize kuwa na fursa ya kushiriki, pia ametuma mwaliko kwa uongozi wa msanii Ali Kiba akibainisha kuwa matamasha ya aina hiyo yanatakiwa kutumika kuondoa tofauti za wasanii.

"Wenzetu (wasanii) Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.” “Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond.