- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DEVOTHA MINJA HOSPITAL MORO HAINA MOCHWALI.
Dodoma: MBUNGE wa Viti Maalum, Devotha Minja (Chadema) amesema kuwa licha ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kuwa ya muda mrefu lakini bado inakabiliwa na changamoto lukuki.
Akichangia katika hotuba ya Wizara Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 Minja amesema hospitali hiyo inaukosefu wa majokofu ya kuifadhia maiti.
Pia amesema hospitali hiyo haina mashine ya X-Ray na iliyopo ni ya kizamani sana ambahyo kwa sasa haikidhi mahitaji.
“Hospitali ya mkoa wa Morogoro inahudumia wagonjwa 500 kwa siku sawa na wagonjwa 15,000 kwa mwezi lakini bado inakabiliwa na chamgamoto mbalimbali,ikiwa ni pamoja na kukosekana jokofu la kuifadhia maiti.
“Kama hiyo haitoshi bado inakabiliwa na ukosefu wa mashine ya mionzi yaani X-Ray,na iliyopo ni ya kizamani na haiwezi kukidhi mahitaji ambayo yanatakiwa kwa sasa” alieleza Devotha Minja.
Akiendelea kuchangia alisema hospitali hiyo pia haina kipimo cha kupimia wingi wa damu ambapo ukienda katika hospitali za watu binafsi kipimo hicho kinapatikana kwa urahisi.
Akizungumzia suala la madaktari bingwa amesema licha ya hospitali hiyo kupokea wagonjwa mbalimbali na hasa wale waliopata ajali, amesema hospitali hiyo haina madaktari bingwa wa mifupa pamoja na chumba cha upasuaji.
Amesema chumba cha upasuaji kilichopo ni kimoja mabacho utumiwa na watu wote bila kijali kuwa wapo wale wanaotakiwa kuhudumiwa vidonda au waliovunjika.
Mbali na hilo alishangazwa na Tanzania kushindwa kuwapatia kipaumbele madaktari wa ndani kwa kuwaboreshea maslahi yao hadi wanafikiria kupata kazi katika nchi ya jirani ya Kenya.
Amesema serikali pia ieleze ni kwanini mpaka sasa hazijajengwa zahanati za kutosha katika kila kata kama ilivyokuwa imekusudiwa na kuna ugumu gani wa kujenga zahanati hizo.
Akiendelea kuchangia pia amesema siyo sahihi viongozi wa Kisiasa hususani Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwakalipia wanataaluma na kufikia hatua ya kuwatumibua bila kufuata utaratibu.
Amesema serikali inatakiwa sasa kujipanga na kuangalia upya ni jinsi gani ya kuweza kulipa madeni yote ya madaktari badala ya kuwaona madaktari hao kama sehemu ya kero.