- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DEREVA WA LORI LA MAFUTA LILOLIPUKA APATIKANA AKIWA HAI
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma nchini Tanzania limesema Dereva wa lori la mafuta ya petroli lililopata ajili baada ya kuacha njia kutokana na kugonga mti Kijiji cha Hangangadinda mkoani Ruvuma nchini Tanzania kisha kichwa cha gari hilo kuwaka moto na kuteketea amepatikana akiwa hai.
Dereva huyo kwa jina la Hubert Mtete mwenye umri wa miaka 40 alikuwa anaendesha Gari aina ya Scania yenye namba za usajili T243 DTV ikiwa na shehena ya mafuta ya petrol lita 33,000 mali ya James Mwinuka ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Njombe Filling station ikitokea Njombe kwenda Songea ilipata ajali huku tenki likisalia pasina kuungua
Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa amesema wamempata dereva huyo na wamechukua jukumu la kufikishwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu zaidi kwani ana michubuko kidogo na amevunjika mbavu.
Kamanda Marwa amesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kufaham chanzo cha ajali hiyo ingawa mafuta lita 33,000 aliyokuwa amebeba yamekutwa salama na mmiliki wa mafuta hayo ameshahamisha kwa msaada wa ulinzi wa polisi na hajalalamika kuibiwa mafuta yake.
Ajali hiyo iliyotokea juzi Jumapili Agosti 11,2019 saa 4 usiku.