Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:51 pm

NEWS: DEREVA WA LISSU KUJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI .

DODOMA: Kufuatia tukio la kupigwa na kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Mh.Tundu Lissu Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limekamata na kuyafanyia uchunguzi jumla ya magari 8 aina ya Nissani Patrol kuhusiana na tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake kamanda wa Jeshi hilo Mkoani hapa Gilles Muroto pia amesema katika msako mkali unaoendelea kufanywa na jeshi hilo wamefanikiwa kukamata watuhumiwa mbalimbali wakiwemo wanaojihusisha na madawa ya kulevya

Aidha pia Jeshi hilo limemtaka Dreva wa Mh.Lissu aliyekuwa naye siku ya tukio ambaye amefahamika kwa jina moja la Adamu pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA Vicent Mashinji kujitokeza na kufika kituo cha Polisi Dodoma au Makao Makuu ya Upelelezi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo

Sambamba na hayo Jeshi hilo limewatahadharisha wanasiasa kujiepusha na matamko yasiyo rasmi na kutotumia tukio hilo kama mtaji wa kujitajirisha kisiasa bali wawe watulivu na wawaachie Polisi wafanye kazi yao

Ikumbukwe kuwa tukio la kupigwa risasi kwa Mh.Lissu lilitokea Septemba 07 mwaka huu majira ya saa saba na nusu mchana huko Area D,katika Maghorofa ya TBA site 3,katika Wilaya na Mkoa wa Dodoma