- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DCB BANK KUWANUFAISHA WANA DODOMA
Dodoma: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene amewataka wananchi kuchangamkia fursa za kimaendeleo zinajitokeza katika mkoa wa Dodoma kutokana na mkoa kuwa makao makuu ya nchi.
Simbachawene amesema Dodoma inatakiwa kuwa kipaumbele kwa wafanya biashara wadogo wqadogo wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Simbachawene ametoa ushawishi huo kwa wafanyabiasha wa mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa tawi la Benki ya DCB commercial Bank uliofanyika katika viwanja vya jengo la LAPF Mjini hapa.
Kutokana na hali hiyo wananchi wametakiwa kuhakikisha wanachangamkia fursa hiyo ili kujikomboa na umasikini ambao unaonekana kuwa kikwazo kwa wananchi waliowengi.
Akizungumzia DCB aliwataka wananchi kujiunga na benki hiyo ili kuweza kufungua akaunti ili kuweza kupata mkopo kwa masharti nafuu pamoja na kutoza riba kidogo ambayo ni miatano kwa mwezi.
Naye mkurungenzi wa DCB commercial bank, Endson Mkwawa amesema lengola Kufungua tawi hilo ni
Kuhudumia wateja na wakazi wa mkoa wa Dodoma.
Kuinua uchumi wa wakazi wa Dodoma.
Mikopo inayotolewa ni.
- Kutoa mikopo ya ujenzi.
- Kutoa mikopo ya ukarabati wa nyumba.
Pia Mkwawa ameeleza kuwa matarajio ya DCB bank ni
- Kupata faida baada ya kodi ya billion 3.2.
- Kuboresha huduma na kujitangaza ili wananchi ili wajue huduma zao.
Uzinduzi huo uliambatana na vikundi mbalimbali vya burudani kama vile Majereko Dodoma.