- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC MTATURU ASISITIZA KULINDA AMANI NA UPENDO
MANYONI: MKUU wa Wilaya ya Ikungi kijiji cha Mwau Kilichopo kata ya Manyoni Miraji Mtaturu amewahasa waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kulinda amani iliyopo, kwa kuwa ndio msingi wa kila jambo ikiwemo maendeleo na ibada.
Mtaturu aliyasema hayo wakati Akihutubia mara baada ya ibada ya swala ya Eid El Hajji iliyofanyika wilayani humo mkoani singida.
Aidha amewataka kuwa wamoja,kupendana na kuishi kama ndugu bila ya kuangalia misingi ya dini wala itikadi za vyama vyao.
Alisema serikali ina amini kuwa waumini wakifuata mafunzo na imani za dini zao watakuwa raia wema na watasameheana pale wanapokeseana.
“Ndugu zanguni tuidumishe na kuilinda amani tuliyonayo,bila ya kuwa na amani hatuwezi kufanya shughuli zozote za kimaendeleo,hatuwezi kushiriki ibada kama hivi,amani ndio kila kitu kwetu,”alisema Mtaturu.
Alisema ili kuilinda amani kila mmoja amuheshimu mwenzie bila ya kuangalia tofauti ya kabila,dini wala chama na kusisitiza kuwa siasa sio uadui na uwepo wa vyama vingi ni kuonyesha namna nchi ilivyo na demokrasia.
“Waumini wenzangu tusiifanye siasa kuwa ni adui,uchaguzi ulishaisha hivyo kwa sasa tunapaswa kuwasaidia wananchi kusukuma maendeleo,hapa katikati tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa wakitoa kauli za kuwagawa wananchi na kuwachonganisha na serikali yao sisi tusifuate kauli zao,zinaonyesha ulimbukeni walionao na kudhoofisha maendeleo,”alisema mkuu huyo.
Alisema walioanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa hawakumaanisha viwepo vyama vya kukwamisha maendeleo hivyo wanasiasa wanawajibu wa kuacha siasa chafu zinazorudisha nyuma maendeleo ya wananchi ili nchi iweze kusonga mbele.
Akizungumzia kuhusu maendeleo wilayani humo amewahamisha wananchi kulima kilimo cha kujitosheleza ili wapate chakula cha kutosha na kuweka bayana mkakati wa wilaya wa kuja na zao la korosho ambapo kwa msimu huu watagawa bure miche laki 5 kwa wananchi.
Kwa upande wake mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)wilaya ya Ikungi sheikh Salum Ngaa alimshukuru mkuu huyo kwa kujumuika nao katika ibada hiyo na kuwahimiza waumini kufanya matendo mema yaliyoaswa na Mungu.
Alisema Hijja ni miongoni mwa nguzo za uislam hivyo imelazimishwa kuitimiza na malipo yake ni makubwa kwa Allah hivyo waislamu wanapaswa kuifanya sikukuu hiyo kuwa kwa ajili ya kufanya yale wanayofanya mahujaji waliopo hijja.
Katika ibada hiyo mh Mtaturu amechangia bati bandari(bati 16)mifuko 10 ya saruji baada ya kukuta kuna ujenzi wa madrasa ya vijana ya kujifunzia unaendelea na umefikia hatua ya upauaji ambapo pamoja nae waumini wengine nao wameunga mkono na kuchanga sh laki 327,950 taslimu huku ahadi ikiwa ni sh 30,000,mifuko ya saruji 7 na bati 14.