- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC MTATURU AENDELEA KUGUSA MAISHA YA WANYONGE.
IKUNGI SINGIDA: Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mh Miraji Mtaturu ameamua kugharamia masomo ya mwanafunzi Faidha Ntandu ya kidato cha tano na sita.
Mwanafunzi huyo amemaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Unyahati na kufaulu kwa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.
Faidha kwa sasa analelewa na mama yake mkubwa Sitta Dude baada ya mama yake mzazi kufariki dunia.
Kutokana na ufaulu huo amepangiwa kujiunga kidato cha Tano shule ya Sekondari Karema wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa mwaka wa masomo 2019/2020.
Akizungumza ofisini kwake na mwanafunzi huyo aliyeambatana na mama yake mkubwa, mh Mtaturu amesema ameguswa na juhudi za mtoto huyo.
“Nakupongeza mtoto wangu kwa kufanya vizuri katika masomo yako,najua changamoto unazozipitia,kama kiongozi wa serikali katika wilaya hii niahidi kuwa nitagharamia masomo yako mpaka utakapomaliza kidato cha sita,”alisema mh Mtaturu.
Amesema serikali inaweka mikakati mbalimbali ya kumlinda mtoto wa kike ili atimize ndoto zake.
"Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu kumsaidia mtoto huyu, tumekuwa tukihimiza kumlinda mtoto wa kike na hilo linaenda sambamba na kumpatia elimu, aliongeza mh Mtaturu.
Akitoa shukrani kwa msaada huo Faidha amemshukuru mh Mtaturu kwa moyo wake huo wa kuwaona na kuwajali wasio na uwezo na kuahidi kufanya vizuri zaiidi katika masomo yake.
#IkungiYetu#ElimuYetu#MaendeleoYetu#