- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC MTATIRO ATAKA VIBOKO KUTAWALA KWA WATORO SUGU
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Julius Mtatiro ameendeleza kampeni ya kiwilaya ya kupambana na utoro sugu, nidhamu za wanafunzi na mimba za utotoni wilayani Tunduru, na leo amewaelekeza walimu kuwaadhibu watoro sugu mbele ya wazazi wao na amezionya pande zote zinazohusika na uzembe huo.
Katika kampeni hiyo Ndg. Mtatiro ameelekeza wazazi wa wanafunzi sugu kwa utoro na watoto wao wajisalimishe kwenye shule zote za Sekondari na Msingi katika wilaya hiyo.
Katika kutekeleza agizo hilo watendaji wa kata, waratibu elimu kata na walimu wa shule zote wameendelea kutoa adhabu kwa wanafunzi hao na kuwaonya wazazi ambao wameshindwa kuwasimamia watoto.
Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Ligoma iliyoko tarafa ya Namasakata Wilayani Tunduru Ndg. Mtatiro amewaonya wazazi wa watoto sugu kwa utoro kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika wilaya nzima ni kali mno dhidi yao.
"Rais Magufuli na serikali yale anatenga Shs Bilioni 23.6 za kitanzania kila mwezi ili msome bure, nyinyi na wazazi wenu mnachekeana na kupuuza masomo, mnalifanya taifa linapoteza fedha nyingi na Rais anahangaika kutumia kodi za watanzania ili watoto wenu wapate elimu wawe na maisha bora lakini mnapuuza juhudi hizo", ameeleza mhe. Mtatiro.
Ndg. Mtatiro amewaelekeza maafisa wote wanaosimamia elimu na utawala katika vijiji na kata za Tunduru kuendelea na msako mkali kuhakikisha watoto wote wanaendelea na masomo na ikibidi wazazi wachukuliwe hatua kali, maelekezo hayo yameanza kutekelezwa na wazazi wengi ambao wanawasalimisha watoro sugu kwenye shule zao.