Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:43 am

NEWS: DC LONGIDO AAGIZA KUKAMATWA KWA MUWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

Longido: Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kumsaka na kumkamata, mkurugenzi wa kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Green Miles Safaris Ltd, Salim Abdalah Awadhi kwa kushindwa kuvilipa vijiji vinavyozunguka kitalu kiasi cha Sh329 milioni.

Picha inayohusiana

Agizo hilo limekuja mara baada ya DC huyo kuzungumza na viongozi wa vijiji na kata zinazozunguka kitalu hicho nakusema Serikali sasa haiwezi tena kumvumilia mwekezaji huyo kutokana na kukaidi kulipa makubaliano yake na vijiji kwa miaka minne. Alisema mwekezaji huyo pia ameshindwa kudhibiti matukio ya ujangili katika kitalu chake kwani ndani ya miezi mitatu mizoga ya Twiga 16 imeokotwa. "Thamani ya Twiga mmoja ni kama Sh30 milioni sasa piga hesabu tumepoteza kiasi gani katika twiga 16 (Sh 480 milioni)," alisema.

Alisema mwekezaji huyo imebainika ana mahusiano mabaya na vijiji hivyo, Serikali ya wilaya itaandika barua rasmi wizara ya Maliasili na Utalii ili ikiwezekana aondolewe. Awali madiwani na wenyeviti wa vijiji alipowekeza mwekezaji huyo, walitoa tamko la kuitaka Serikali kumuondoa mara moja kabla ya kusababisha migogoro zaidi. Diwani Alayce Moshau wa kata ya Mdarara na Timotheo Laizer kata ya ya Ketumbeini walisema hawamtaki mwekezaji huyo kwani ameshindwa kutimiza matakwa ya mkataba wake