- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC IRINGA AFAFANUA KAULI YA KUWATENGA WATU WA DAR
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ametoa ufafanuzi juu ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ya kuwa wananchii wa Iringa wahakikishe wasikae karibu kabisa na watu wanaotoka Dar es salaam, akifafanua kuwa kauli yake hiyo ililenga mazingira ya msibani alipokuwepo kutokana na kutokea kwa vifo viwili mfululizo ndani ya msiba mmoja.
Akiongea leoAprili 19, 2020 na kituo cha Azam Tv Kasese amesema kuwa hawatengi wala kumnyanyapaa mtu yeyote kutoka mkoa wa Dar es salaam bali alitaka kuwatahadharisha wakazi wa iringa kwa nia njema kabisa
"Tulikuwa na Msiba hapa zilikuja Tx mbili, zilikuwa zimebeba watu wengi wamejazana, katika msiba huo siku hiyohiyo usiku wake akafa mtu mwingine, kwahiyo walikufa watu wawili katika nyumba moja, kwahiyo tukachukua mazingira ya kujiangalia zaidi" amesema Bw. Kasesela.
Kasesele ameongezea kusema kuwa hajaweka katazo la mtu yeyote kutoka Dar es salaam kuingia Mkoani Iringa bali alitoa tahadhari kwakuwa watu wengi kutoka Dar es salaam hawapimwi juu ya maambukizi ya Ugonjwa huo.