- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DAR ES SALAAM YAONGOZA KUWA NA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA
DODOMA: MKOA wa Dar-es-Salaam unaongoza kwa kuwa na waathirika wengi wa dawa za kulevya ukilinganisha na mikoa mingine.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto KHAMIS KIGWANGALA wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum MGENI JADI KADIKA.
Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua ni mkoa gani unaoongoza kwa kuwa na waathirika wengi wa dawa za kulevya na serikali ina mpango gani ya kutoa matibabu bure kwa waathirika hao.
Dokta KIGWANGWALA amekiri kuwa ni ukweli usiopingika kuwa kuna wimbi kubwa la ongezeko ya matumizi ya dawa za kulevya katika sehemu mbalimbali nchini.
Amesema matumizi ya dawa za kulevya yameongezeka hasa katika mikoa mikubwa ikiwemo Dar-es-Salaam, Tanga, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Kutokana na hilo amesema Wizara inaendelea kutoa huduma kwa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya bure katika vituo mbalimbali vya umma vinavyotoa huduma hiyo na hivi Wizara imefungua vituo katika Hospitali ya Muhimbili, Mwananyamala, na Temeke kwa Mkoa wa Dar-es-Salaam.