- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DAKTARI 'FEKI' WA MUHIMBILI ,ANASWA TENA HOSPITALI YA AMANA
DAR ES SALAAM:Baada ya miezi mitatu juni 19 mwaka huu kupita Abdallah Juma mkazi wa jiji la Dar es salaam kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiwa katika maabara kuu akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana.
Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.
Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU), Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Alisema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa watu waliokuwa wakihitaji huduma katika hospitalini hiyo.
Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.
Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.
Nae mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia alisema Agosti 9 mwaka huu, kijana huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi katika hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo anaweza kuwasaidia.
“Alituambia kuwa fomu zinatolewa katika hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia.
Aliongeza,Juni 19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.
“Tuliamua kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa leo ,”alieleza.