- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DAKTARI ALIYEOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI
Zanzibar: Wizara ya afya visiwani Zanzibar imemsimamisha kazi Daktari wa Hospitali ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba, Massoud Sleiman Abdalla akituhumiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mwanamke mjamzito alikwenda kupata patibabu hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Novemba 26,2019, Waziri wa afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed amesema wamefanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
Amesema wamepokea barua kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi (ZAECA) yenye maelezo kuhusu kukamatwa kwake hivyo wamelazimika kufuata taratibu za kazi ikiwemo kumsimamisha kazi.
Amesema licha ya daktari huyo kukamatwa kwa tuhuma hizo haimaanishi kila mtaalamu wa afya ndiyo tabia zao kwani huenda wakawapo wachache wenye dhamira ya kuichafua kada hiyo.
Awali, Mkurugenzi utumishi na uendeshaji wa wizara hio Ramadhan Khamis Juma amesema kwakuwa mtuhumiwa amekamatwa kwa hatia hyio hawana budi kufuata sheria za kazi.