- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DADA WA GANAVA BALALI AFUTIWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imekubali kumfutia kesi ya uhujumu uchumi dada wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, marehemu Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuomba kuifuta kesi hiyo.
Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumanne Arili 14, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuwasilisha maombi ya kuondoa mashtaka baada DPP kuona haoni haja ya kuendelea nalo.
Hakimu Isaya alikubali maombi hayo na kuamuru kesi iondolewe na mshtakiwa aachiwe huru katika shauri hilo.
Mshtakiwa huyo alikuwa anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam alijipatia kiasi cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Roderick Kisenge kwa ulaghai.
Inadaiwa alijipatia fedha hizo baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambazo halijapimwa lililopo eneo la Boko Dovya Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.
Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa katika kipindi hicho mshtakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo katika Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya kufutiwa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo alifunguliwa mashtaka mapya ambapo alirudishwa mahabusu akisubiri kusomewa.