- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CUF MAALIM SEIF YATEUWA WAJUMBE WAPYA BODI YA WADHAMINI
Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wamefanya uteuzi wa wajumbe wanane wa bodi ya wadhamini baada ya kukutana jana Jijini Dar es salaam.
Wajumbe walioteuliwa kujaza nafasi za wajumbe wa bodi hiyo ya wadhamini ni pamoja na Abdallah Khatau, Ali Mbaraka Suleiman, Yohana Mbelwa na Mohamed Nassor Mohamed.
Wengine ni Dk. Juma Ameir Muchi, Zumba Kipanduka, Mwanawetu Zarafi, Mwana Masoud Ali na Blandina Mwasabwite.
Uwamuzi wa chama hicho kuteuwa wajumbe hao imekuja siku chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji enhajj Masoud, kutengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya upande ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, vilelevile Jaji Masoud alisema hata wajumbe wa upande wa Maalim Seif waliokuwa wamependekezwa, nao hawatambuliki kwani wamekosa uhalali kisheria.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob kama Ofisa kutoka Mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya The Trustees incorporation Act. CAP 318 RE: 2002 Section 17(1).
Pia kikao hicho kilimwalika Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia.
“Kikao kilikuwa na ajenda moja pekee ambayo ni kujaza nafasi za wajumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF, ambapo wajumbe 37 walihudhuria kati ya wajumbe wote 63 kama wangekuwepo kama walivyochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa mwaka 2014.
Na hivyo kufanya kupatikana (koramu) ya zaidi ya nusu ya wajumbe halali waliopaswa kuhudhuria kikao hicho” ilieleza taarifa hiyo.