- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CUF MAALIM SEIF WAUNGA MKONO LIPUMBA KUZUIWA KUFANYA MKUTANO
Dar es Salaam. Wanachama wa chama cha wananchi CUF upande wa Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif wa kata ya Azimio wamesema wanaunga mkono tamko la katibu mkuu huyo la kuzuia mkutano uliopangwa kufanywa na kambi ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Prof. Lipumba wenye lengo la kumfukuza Maalim Seif uanachama,
Akizungumza kwa niaba ya wanachama katibu wa kata hiyo, Rajabu Matata amesema wanapinga kwa nguvu zote mkutano feki wa Lipumba anaouita mkutano mkuu wa taifa unaotokana na wajumbe feki. "Sisi tukiwa wanachama tawi la Be Care hatujawahi kuona uchaguzi unaendeshwa kwa ngazi ya matawi, kata au wilaya kwa lengo la kupata wawakilishi wa taifa," amesema Matata.
Amesema wanataka utaratibu ufanyike kama unavyofanyika kwa miaka yote na kuviomba vyombo vya dola kuzuia mkutano huo feki, wasipofanya hivyo viongozi na wanachama watahakikisha wanatumia njia wanazozijua wao. Hassan Malenga ambaye ni mwanachama wa tawi la Be Care amesema maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu Maalim Seif wameyapokea na wameanza kuyatekeleza kukabiliana na wajumbe feki wa mkutano huo