- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CUF "MAALIM SEIF'' HAIWATAMBUI WABUNGE WALIOAPISHWA JANA
Dar es salaam: Chama cha wananchi CUF Upande wa maali Seif kimesema hakiwatambui wabunge walioapshwa Jana Bungeni na spika wa Bunge Hilo Job Ndugai kwa kuwa si wabunge halali wa chama hicho , akiongea na waandishi wa habari leo Septemba 6 Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa CUF, Mbarala Maharagande amesema kuwa bado wanawatambua wabunge wanane waliovuliwa uanachama hivyo kupoteza ubunge.
Amesema Baraza Kuu la Uongozi la CUF linaendelea kuwatambua wabunge na madiwani waliovuliwa uanachama kwa kuwa bado ni wanachama halali wa chama hicho.
Maharagande amemtupia lawama Spika Job Ndugai akidai analitumia Bunge vibaya kukandamiza upinzani.
Amesema bunge linapaswa kuwa chombo muhimu cha Watanzania katika kuisimamia Serikali ili wananchi wapate maendeleo.Wabunge walioapishwa jana Septemba 5 wanachukua nafasi ya wenzao waliofukuzwa uanachama na Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ni mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.