Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:16 pm

NEWS: CORONA YAWASILI TANZANIA MGONJWA MMOJA APATIKANA MOSHI

Mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya Corona amegundulika katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha-Waziri wa Afya Ummy Mwalimu athibitisha.

Mgonjwa huyo ambaye ni Mwanamke (46) raia wa Tanzania ametokea nchini Ubelgiji Machi 15, 2020 na kwasasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mawenzi, mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Image result for corona africa

"Alipokuwa Ubelgiji nyumba aliyofikia Mume wa mwenye nyumba aliugua corona, Airport KIA hakubainika kuwa na homa ila alijishuku akaenda kujifungia Hotelini, baadae akaenda Mount Meru Hospitali, sampuli ilichukuliwa hadi Maabara na imethibitika ana Corona” amesema Ummy

Image result for corona africa

Leo Machi 16 Hospitali ya Taifa Muhimbili na taasisi zote za hospitali hiyo kuanzia leo Machi 16 wataruhusu ndugu wawili asubuhi na jioni huku mmoja akiruhusiwa mchana kuona ndugu zao wanaopatiwa matibabu ili kuchukua tahadhari ya kusambaa kwa virusi vya corona

Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kimeripotiwa nchini Kenya juzi Machi 13 mwaka huu. Wizara ya Afya nchini humo imesema kuwa kisa hicho kilithibitishwa siku ya Alhamisi kwa raia wa taifa hilo aliyesafiri kutoka Marekani akirejea nyumbani. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema mgonjwa huyo amewekwa kwenye karantini na yuko katika hali nzuri. Sikiliza ripoti ya Shisia Wasilwa.

Hiki ni kirusi cha aina gani?

Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji. Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19.

Image result for corona africa

COVID-19 ni nini?

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Dalili za Corona ni zipi?

Dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Lakini isikutishe, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

Makundi yaliyo kwenye hatari zaidi ni yapi?

WHO inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama Shinikizo la Damu, Kisukari, Matatizo ya Figo ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kuathika pindi wanapopatwa na virusi vya Corona. Watu wa umri wa wastani na wenye afya imara wanaweza kupata virusi vya Corona na kupona bila kuhitaji matibabu.