Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:29 am

NEWS: CORONA YABADILI UTARATIBU WA KUINGIA KWENYE MWENDOKASI

Dar es Salaam. Shirika la Usafiri wa Mwendokasi (DART) Jijini Dar es salaam limeanzisha utaratibu mpya wa kuingia kwenye mabasi kwa kufuata foleni mbili; moja ya wanawake na nyingine ya wanaume na kwa idadi ambayo inapunguza mgusano wa abiria ili kuweza kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa tishio Duniani.

Hii ni Baada ya Tanzania kuripotiwa watu sita kuugua ugonjwa wa corona, abiria wanaotumia usafiri wa mwendokasi kutoka Kimara Mwisho kwenda Gerezani, Morocco na katikati ya Jiji la Dar es Salaam wanalazimika kupanga foleni ili waweze kupanda magari hayo.

Utaratibu huo wa foleni umeanzishwa leo Ijumaa Machi 20,2020 Kampuni ya Mwendokasi.

Abiria hao baada ya kushuka katika magari hayo hulazimika kupanga mistari kwa ajili ya kunawa mikono au kupaka vitakasa mikono (Sanitizer).

Katika eneo hilo, kuna njia mbili , abiria anaamua anawe mikono au apake kitakasa mikono.

Baada ya hapo anaingia upande wa pili kwa ajili ya kupanda gari kwenda sehemu anayoenda.