Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:33 pm

NEWS: CONGO YAIDHINISHA ELIMU BURE KWA SHULE ZA UMA

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo leo inaingia katika tukio la kihistotia kwa kuidhinisha elimu ya bure katika shule za msingi za umma kwa lego la kutekeleza yaliomo katika katiba ya mwaka 2005, ambayo inasisitiza elimu ya bure kwa watoto wa shule za msingi.

Kumekuwepo kwa utaraitubu wa Tangu mwaka 1993, wazazi ndio wakilipa walimu ada ya mafunzo na hivi sasa serikali imeamua kuwalipa mishara.

Lakini baadhi ya walimu mpaka sasa wana shaka kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo mpya ya serikali.

Walimu wanatishia kuanza mgomo ikifika tarehe ishinirini mwezi huu ikiwa serkali haitawalipa mshara wa kutosha.


'Amechukuwa (Felix Tshisekedi) hatua hio ya kusema wazazi wasilete tena pesa, sisi tumemunga mkono, hapa kwani nina walimu ambao hawajawahi kupokea pesa kutoka kwa serkali, nadhani ni muhimu kulipa walimu ,kama walimu hawatalipwa haraka, itakuwa athari sana' amesema Moju.

Gharama ya elimu ya bure kwa watoto wa shule ya msinigi ni kama 40% ya bajeti ya nchi ambayo ni ya dola za Marekani karibu bilioni sita.

Wachambuzi wa uchumi wana shaka iwapo hatua hio ya serikali itafanikiwa lakini rais Felix Tshisekedi ana matumaini mengi.

"Itakuwa hatua ambayo itakamilishwa katika miezi michache ijayo. "Mpango huu tumeukuta lakini hakukuwa na bajeti. Hili ndilo nitakalolipa kipaumbele. Congo ina uwezo wa kuongeza mshahara kugharamia elimu na tutalipa" amesema rais Felix tshisekedi.

Serikali mpya ilihiadi kufuatiliwa kwa karibu pia uamuzi huu wa rais wa kutoa elimu ya bure kwa watoto wa shule za msingi.