Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:32 am

NEWS: CHINI YAITAKA MAREKANI KUONDOA MUSWADA WA HONG KONG

Wizara ya mambo ya kigeni ya China imemuita balozi wa Marekani kuitaka Marekani iondoe sheria iliyopitishwa bungeni ikiunga mkono vuguvugu la maandamano ya kudai demokrasia mjini Hong Kong, la sivyo italazimika kupambana na hatua kali.

Image result for Zheng Zeguang against U.S"

Mswada wa Hong Kong unaosubiri kutiwa saini na rais Donald Trump unaunga mkono haki za binadamu na demokrasia katika mji huo, wakati ukitishia kuondoa hadhi maalum ya eneo hilo ya kiuchumi.

Image result for Zheng Zeguang against U.S"

Hatua nyingine inapiga marufuku uuzaji wa mabomu ya kutoa machozi, risasi za mipira na vifaa vingine vinavyotumiwa na majeshi ya usalama kukandamiza maandamano ya kudai demokrasia.

Wizara hiyo imesema Naibu waziri Zheng Zeguang amemwita balozi wa Marekani Terry Branstad jana Jumatatu kuelezea upinzani mkali kuhusiana na mswada huo.Trump hajaonesha ishara iwapo atatia saini mswada huo kuwa sheria, akisema wiki iliyopita kuwa wakati akiwaunga mkono watu wa Hong Kong , pia anamuunga mkono rafiki yake rais wa China Xi Jinping.