Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:25 pm

NEWS: CHINA YALAANI KIONGOZI WA MAANDAMANO HONG KONG KUZURU UJERUMANI

China imelaani vikali hatua ya Ujerumani kumruhusu mwanaharakati wa Hong Kong Joshua Wong kuzuru nchini Ujerumani.

Katika tamko lake wizara ya mambo ya nje ya China imesema nchi hiyo haikuridhishwa hata kidogo na uamuzi wa Ujerumani wa kuwaalika wale wanaotaka kujitenga na wanaoshiriki katika harakati dhidi ya China.

China pia imewasilisha malalamiko rasmi juu ya mkutano baina ya waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas na mwanaharakati Wong. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying ameeleza kuwa ni makosa makubwa kwa vyombo fulani vya habari vya Ujerumani na wanasiasa kujipatia mtaji wa kisiasa kwa kusimama kwenye jukwaa moja na wale wanaoendesha harakati za kujitenga dhidi ya China.

Hatua hizo ni kudharau uhuru wa China na pia ni kujiingiza katika mambo yake ya ndani. Hata hivyo Ujerumani imeyapinga malalamiko hayo. Katika ziara yake ya China wiki iliyopita Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema Ujerumani inaunga mkono sera ya nchi moja na mifumo miwili tofauti.